Wednesday , 4th Jun , 2014

Serikali ya Tanzania imesema kiwango cha umasikini wa mahitaji ya msingi kwa Tanzania Bara kimeendelea kuwa chini kwa asilimia 28 ikiwa ni pamoja na uhitaji wa chakula kwa wakazi wa mijini.

Waziri wa fedha na uchumi Bi. Saada Mkuya Salum.

Hayo yameelezwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum wakati akielezea namna ambavyo serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini Mkukuta katika hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015.

Awali wakati wa maswali na Majibu,Naibu Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI ,anayeshughulikia Elimu, Mhe Kasim Majaliwa wakati akijibu maswali ya wabunge amesema walimu 33,894 kati ya walimu 36, 186 waliopangwa kuajiriwa na serikali mwaka jana wameripoti katika vituo vyao vya kazi na kupunguza uhitaji wa walimu.