Wednesday , 9th Nov , 2016

Takribani tani bilioni 1.3 za chakula hupotea kila mwaka , huku watu wapatao bilioni moja wakikabiliwa na njaa duniani.

Wachuuzi wa mazao ya chakula wakiwa

 

Hayo ni kwa mujibu wa makadirio ya shirika la chakula na kilimo FAO na kamisheni ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya uchumi barani Ulaya UNECE.

Makadirio yao yanaashiria kwamba hasara za kiuchumi zitafikia dola bilioni 940 kwa mwaka kutokana na upotevu huo wa chakula, wakisisitiza kwamba endapo upotevu huo wa chakula ungekuwa nchi, basi utoaji wa hewa chafuzi ungeifanya nchi hiyo kuwa ya tatu duniani.

Kwa mujibu wa FAO/UNECE, wamesesema sababu kubwa ya upotevu wa chakula, imebainika watu wengi hawaangalii tarehe za mwisho wa kutumia bidhaa wanunuazo na matokeo yake nyingi huishia mapipani kama taka zilizoharibika.

Mashirika hayo yameandaa mkutano utakaofanyika Novemba 10 Geneva Uswis ukiwaleta pamoja wadau wa sekta ya chakula, wanaharakati na wataalam wa masuala ya chakula ,ili kubaini changamoto na maeneo muhimu ya kuyachukulia hatua kuzuia ongezeko la upotevu wa chakula.