Watu hao wameandika kwenye mitandao ya kijamii maoni yao juu ya shirika hilo ambalo limeonekana kuwa moja wa vitu vinavyorudisha nyuma na kukwamisha shughuli za uzalishaji mali, huku wakilalamika kuwa haliwatendei haki.
EATV ilifanya jitihada za kuwatafuta wahusika wa Tanesco ili kulizungumzia hilo lakini haikufanikiwa kuwapata kwa mara moja, na badala yake Tanesco ilijibu hoja za wananchi kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa twitter ikisema tatizo la kukatika kwa umeme limetokana na kugundulika kuwa mifumo ya gridi ya taifa haijatengemaa vizuri, hivyo mafundi wanaendelea na kazi kuhakikisha huduma ya umeme inarejea.
Soma hapa chini baadhi ya maoni ya watu walioandika kuhusu Tanesco.