Saturday , 28th Jun , 2014

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA) kimeanza kampeni ya miaka mitatu ya kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinavyochangiwa na tabia ya ulevi.

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini Tanzania

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA) kimeanza kampeni ya miaka mitatu ya kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinavyochangiwa na tabia ya ulevi.

Akiongea leo na wahariri wa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa Bi. Valerie Msoka amesema kwa kuanzia kampeni hiyo itafanywa katika Wilaya ya Kinondoni.

Bi. Msoka amesema kuwa ulevi umekuwa ni chanzo kikuu cha ukatili wa aina mbalimbali katika ngazi ya familia ukiwemo ukatili wa kingono unaofanywa kwa wanawake na watoto.

Takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kuwa asilimia 77 ya matukio ya ukatili wa kingono yalichangiwa na ulevi huku asilimia 33 yakiwa hayahusiani na ulevi.