
Akizungumza katika ziara yam bio za Mwenge ambapo kwa sasa upo mkoani Manyara Afisa Uchunguzi wa TAKUKURU Safieli Mshana amesema idara yake imepokea malalamiko 150 kutoka kwa wananchi huku mahakama na serikali za mitaa zikiongoza.
“Tumepokea malalamiko 150 na hii inaonyesh amwitikio wa wananchi katika kuripoti matukio ya rushwa tofauti na kipindi cha huko nyuma” Amesema Mshana.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa George Mbijima amewataka watendaji wa serikali kuridhika namishahara yao katika kuwatumikia watanzania.