Baadhi ya viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakijadili moja ya vipengele tata katika rasimu ya pili ya katiba.
Katibu mkuu wa chama hicho ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba Bw. Juma Ali Khatib, ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam ikiwa imebakia siku chache kabla ya kuanza kwa vikao vya bunge hilo ambavyo vilisitishwa kwa muda kupisha bunge la bajeti.
Bw. Khatib amesema hoja wanazozitoa wajumbe wa UKAWA ni za msingi ambazo hata yeye anaziunga mkono lakini njia inayotumiwa na wajumbe hao kutoka vyama vya CUF na CHADEMA sio sahihi kwani suluhu haifikiwi tofauti zinaweza kupatikana ndani ya bunge hilo na hata kwa njia ya mazungumzo.
Amewataka wajumbe hao kutoka UKAWA kutanguliza maslahi ya taifa mbele badala ya yale ya kwao binafsi, sambamba na kuhakikisha kuwa amani inatawala katika mchakato mzima wa upatikanaji wa katiba mpya.