Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Akizingumza leo Bungeni katika kipindi cha Maswali ya Papo hapo kwa Waziri Mkuu,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amekiri uwepo wa uhaba wa sukari lakini sio ambao unaweza kufanya wafanyabiashara kupandisha bei ya sukari hali ambayo inawaumiza wananchi.
Waziri Majaliwa amesema wametoa vibali kwa wafanyabiashara wa viwanda vya sukari kuagiza sukari hiyo ili kuvilinda viwanda vya ndani vya sukari viweze kuendelea na uzalishaji na kudhibiti uingizaji wa sukari holela ambao unafifisha viwanda yao.
Waziri Mkuu ametumia nafasi hiyo kuwasii wafanyabiashara kutopandisha bei ya sukari kwa kuwa kwa kufanya hivyo kunawaumiza wananchi wa hali wakati suala bado halijakua kubwa kiasi cha kuwapelekea kupandisha bei.
Ameongeza kuwa pengo la tani laki moja ambazo zinahitajika tayari wamesashaanza kufanya utaratibu wa uagizaji ili kuziba pengo hilo na kila mwananchi aweze kununua sukari kwa bei elekezi ya 1800.