Thursday , 10th Apr , 2014

Mamlaka ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini Tanzania, inakamilisha taratibu kwa ajili ya kuja na mfumo mmoja wa kukokotoa kiwango cha mafao kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini Tanzania SSRA Bi. Irene Kisaka

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Bi. Irene Kisaka, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kimataifa wa masuala ya fedha, bima na hifadhi ya jamii uliokutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC.

Bi. Kisaka amesema, ujio wa mfumo huo utamaliza mbinu chafu ambazo baadhi ya mifuko ya hifadhi inazitumia kwa ajili ya kusajili wanachama wapya na kitendo ambacho amesema ni kinyume na sheria ya usimamizi wa huduma za hifadhi ya jamii nchini.

Aidha Bi. Kisaka ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kushindana kwa kuboresha utoaji huduma kama vile kupunguza muda wa mwanachama kupata mafao pamoja na kuboresha mafao ya muda mfupi yakiwemo mafao ya matibabu elimu pamoja na huduma.