Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Visiwani Zanzibar. Juma Duni Haji.
Kauli hiyo ya uvunjanji wa mkataba huo uliokuwa wa miaka kumi umetangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miondombinu na Mawasilaino wa Zanzibar Dr. Juma Malik wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea hatua hiyo ya serikali ambapo amesemea kampuni hiyo yenye ofis yake ndogo Dubai imekuwa ikienda kinyume na makubaliano kwa kusajili meli kiholela bila utaratbi ikiwa ni pamoja na kwenda kinyume na jumuiya za kimataifa huku pakiwa na taarifa za kusajili meli ambazo zinahusika na usafirishaji wa Dawa za Kulevya.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Mhandisi Abdi Omari amesemea mamlaka sasa imeamua kufanyakazi hizo wenyewe kwa kushirikiana na wadau wao na kwa sasa pamoja na kampuni hiyo kukataa kukabidhi hati zote za usajili ikiwemo usajili wa meli zaidi ya 350 hakuna hofu yoyote kuhusu mkataba huo huku pakiwa na kipengele cha kulipa dola laki tano kwa uvunjanji wa mkataba ,na kuongeza kuwa serikali ipo tayari kwenda kwenye ngazi za kisheria kuhalalisha uvunjwaji wa mkataba huo..
kampuni ya phioltex ilisaini mkataba wa miaka 10 na SMZ na bado miaka miwili kumalizika kwa mkataba huo na tasisi hiyo ilihusika kusajili meli za mafuta zaidi ya 32 za Iran kinyume na uamuzi wa jumuiya za kimataifa hali iliyosabaisha kuzuka kwa mvutano mkubwa kati ya Tanzania na nchi wahisani..