Friday , 5th Aug , 2016

Mkoa wa Simiyu umeanza mpango wake wa utekelezaji wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwa shule za msingi na sekondari kwa kutenga asilimia 2 ya mapato yanayotokana na zao la Pamba katika halmashauri zote za wilaya ya Mkoa huo.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka.

Akizungumza na Kamati ya Fedha ya Halmashauri za Wilaya Mkuu wa Mkoa huo, Anthony Mtaka, amesema kuwa kutokana na mpango huo kilichobaki hivi sasa ni kuzungumza na kamati za mabaraza ili kuanza rasmi miradi hiyo.

Mhe. Mtaka amesema kuwa kwa licha ya kubaini kuwepo kwa miradi hewa katika halmashauri zao lakini suala hilo linatakiwa kupewa uzito wa juu katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato wa zao hilo la pamba unaleta tija kwa wakazi wa mkoa huo.

Hapo awali madiwani hao walionyesha kuwa na wasiwasi wa mpango huo kutokana na kutokuwa na uwiano sawa wa ulimaji wa pamba katika Halmshauri zao hali itakayopelekea wengine kuonewa katika kutoa pesa hizo.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka,