,Mgombea wa jimbo la Simanjiro kwa tiketi ya CHADEMA ,James Ole Milya.
Akizungumza katika mkutano wa Kampeni,Mgombea wa jimbo la Simanjiro kwa tiketi ya CHADEMA ,James Ole Milya amesema kuwa iwapo UKAWA wataingia madarakani watatunga sheria za kuhakikisha kuwa asilimia 50% ya mapato yanayotokana na madini yatabaki nchini kuchochea maendeleo tofauti na hali ilivyo sasa mchango wa madini kwa pato la taifa ni finyu.
Mwenyekiti Mstaafu wa BAVICHA wilaya ya Arusha mjini,Noel Olevaroya amesema kuwa kimama wa jamii ya kimasai wamekua wakipata shida kutokana na matatizo ya ukosefu wa maji huku wakilazimika kutembea muda mrefu kutafuta huduma hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kata ya Loibor-Siret David Mollel amewataka Watanzania kujitokeza katika uchaguzi Octoba 25 mwaka huu kwani uchaguzi huo utaamua hatma ya maisha ya watanzania na mustakabali wa taifa kwa ujumla katika Nyanja za uchumi,siasa na kijamii.
Wilaya ya Simanjiro ni wilaya inayokaliwa na wafugaji wa jamii ya wamasai ambao hutegemea shughuli za ufugaji kwa kiasi kikubwa kama chanzo kikuu cha mapato mbali na kilimo na shughuli za uchimbaji wa madini aina ya Tanzanite yanayopatikana katika mji mdogo wa Mererani.