Wednesday , 11th Mar , 2015

Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere amesema baada ya kupokea taarifa za kuzushiwa amefariki dunia juzi hakushtushwa na uvumi huo badala yake alifanya sala.

Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam amewathibitishia Watanzania kuwa bado yupo hai na yote hayo amesema anaamini ynatokana na vuguvugu la cuhaguzi mkuu pamoja na utawazi wa sayansi na Teknolojia.

Mama Maria amesema amepokea simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakitaka kumjulia hali akiwemo mkuu wa Majeshi Mstaafu David Musuguri na kwamba alipata usumbufu na kuamua kutokupokea simu za watu wengine.

Kwa upande mwingine mama Maria Nyerere alizungumzia suala la mwanae Makongoro Nyerere Kugombea urais amesema kama raia wa Tanzania mwanae huyo ana haki ya kugombea Urais.

Wiki iliyopita Makongoro alikiambia Chombo kimoja cha Hbari kuwa uamuzi wake wa Kugombea kuwania kiti hicho utajulikana mara baada ya Kamati kuu ya CCM itakaporuhusu kuanza mchakato huo.