Monday , 20th Jun , 2016

Shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini Tanzania (SIDO) limewataka wajasiriamali wa kitanzania kupeleka bidhaa zao ili waweze kutafutiwa masoko ya kimataifa.

Akiongea na East Africa Radio Mkurugenzi mkuu wa SIDO Mhandisi Omary Bakari amesema kuwa kuna wageni wengi toka nje ya nchi ambao huja nchini kwa lengo la kununua bidhaa zinazozalishwa na wajasiliamali wadogo lakini shirika hilo hukosa bidhaa za kuwaonesha .

Aidha Tanzania imetajwa kuwa nabidhaa bora zitokanazo na ngozi hususan viatu hali inayowavutia wafanyabiashara toka nje hivyo ni wakati sasa wa wafanyabiashara wa viatu kuchangamkia masoko ya kimataifa.

Aidha shirika linawahimiza wajasiriamali kuwa na tabia ya kwenda kupata ushauri wa kitaalam ili waweze kuzalisha bidhaa ambazo zinakuwa na ubora unaotakiwa kimataifa.