Saturday , 25th Jun , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu ili kutokomeza matukio ya uhalifu na kuiweka nchi salama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiongea katika uzinduzi wa uboreshaji wa jeshi la Polisi.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa uboreshaji wa jeshi la polisi uliofanyika Kinondoni katika viwanja vya Biafra, Rais Magufuli amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka jana takwimu zinaonyesha matukio ya uhalifu hasa wilaya ya Kinondoni yameongezeka hivyo yanapaswa kudhibtiwa.

Rais Magufuli amesema ili kuhakikisha mfumo huo unaenea kwa haraka nchini nzima atasaidia kuimarisha maslahi ya askari wa jeshi hilo pamoja na kuwaongezea vifaa vya ulinzi ili zoezi hilo liwe lenye tija zaidi.

Aidha, rais Magufuli ametumia fursa hiyo kulionya jeshi la polisi juu ya matumizi ya fedha za umma jambo ambalo limelitia doa jeshi hilo hivyo hawanabudi kujirekebisha ili kurudisha imani kwa Wananchi.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba wakati akiongea katika uzinduzi huo amesema kuwa wanafanya jitihada ya kueneza mpango huo wa maboresho ya jeshi la ili kupunguza zaidi matukio ya uhalifu.

Sauti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli,