Tuesday , 5th Jul , 2016

Shindano la Masoko ya Mitaji na dhamana kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na taasisi za elimu ya juu imezinduliwa huku wanafunzi wakitakiwa kushiriki ili kuongeza uelewa kuhusu masuala ya mitaji ya masoko na dhamana.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko, Mitaji na Dhamana (CMSA), Nasama Masinda.

Akizungumzia shindano hilo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nasama Masinda, amesema analenga kuongeza weledi na ufahamu wa masoko ya mitaji kwa wanachuo.

Massinda amesema pia itasaidia kuongeza washiriki wenye weledi katika masoko ya mitaji na ambao watashiriki kwa kuzingatia kwa kuzingatia sheria na taratibu za ushiriki katika masoko.

Aidha, Ofisa huyo amesema shidano hilo linalenga kuongeza wigo wa wawekezaji kwa kutoa elimu ya kuweka akiba kwa njia endelevu na kuhamasisha matumizi ya TEHAMA.