Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella
Shigella ametoa kauli wakati wa kikao kazi alichokifanya na makatibu Tawala, Wakurugenzi, maafisa utumishi, na watunza hazina wa halmashauri 11 zilizopo Mkoani Tanga.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema watumishi wote watakaopewa mamlaka na majukumu ya kukusanya kwenye vyanzo vya mapato vya halmashauri wawe waadlifu na yoyote akatake bainika kufanya ubadhilifu ni lazima achukuliewe hatua za kinidhamu ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza suala la ukusanyaji wa mapato kwa njia ya Kieletroniki ambapo amesema kuanzia Agosti mosi kila Halmashauri ihakikishe mapato yote yanayokusanywa yanatumia mashine za EFD'S
Wakizungumzia mara baada ya kikao hicho baadhi ya wakurugenzi wameelezea namna ya walivyojipanga katika suala la ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ingawa wamesema ingawa hata mfumo huo wa Elektroni unachangamoto ila wataimarisha ufuatiliaji.