
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori.
Mwenyekiti huyo pia amesema kuwa sheria hiyo itaanzisha migogoro na wananchi.
Akiongea na East Africa radio leo jijini Dar es Salaam, amesema kwa mujibu wa ILO inatakiwa idadi ya Majanga yaendane na mafao yatolewayo na mifuko ya hifadhi ya jamii huku Tanzania ikiwa na majanga takribani tisa wakati idadi ya mafao yakiwa hayajafikia idadi hiyo ya majanga.
Lufulondama ametoa wito kwa serikali kutumia watalaam zaidi kuhusu suala hilo ili wapate njia nyingine mbadala ambayo itatoa afueni kwa wanachama ambao watakuwa wanataka kujitoa katika mifuko hiyo ya kifadhi ya Jamii.
Aidha ameongeza kuwa kulingana na mabadiliko ya kimazingira hata umri wa kuishi nchini Tanzania unapungua kwa mujibu wa takwimu hivyo sheria hiyo ikiwekwa itafanya wanachama wao wengi wasifaidi mafao yao.