Wednesday , 25th May , 2016

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imekiri kuwepo kwa changamoto nyingi kwenye ushirika wa tumbaku nchini hali inayopelekea wizara hiyo kuunda sheria mpya ya ushirika ili kabiliana na changamoto hizo.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha.

Akizungumza bungeni jana Mjini Dodoma katika kipindi cha maswali na Majibu, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha, alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ubadhirifu katika vyama vya madeni makubwa, tozo, makato mengi na usimamizi hafifu.

Mhe. Ole Nasha ameyataja baadhi ya mrekebisho hayo ikiwa ni pamoja na kutumia sheria mpya ya viongozi wabadhirifu katika vyama vya ushirika kuchukuliwa hatua jambo ambalo litawanufaisha wanachama na wakulima wa tumbaku.

Amesema tangu kuanza kwa sheria hiyo hatua zaidi zimechukuliwa katika vyama vya ushirika vya korosho kwa vingozi na watendaji 822,kupewa hati za madai ikiwa pamoja na kufikishwa mahakamani.