
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa Salum.
Hayo yamezungumzwa leo jijini Dar es Salaam, na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa Salum wakati akizungumzia sherehe za mwaka mpya wa kiislam na kusema vijana wakijitambua na kuacha kuiga mambo ya kimagharibi basi taifa litapiga hatua za haraka za kimaendeleo.
Sheikh Salum, amesema vijana wanatakiwa kuhakikisha wanajipanga kwa ajili ya kutumikia jamii yake na taifa kwa ujumla kwa kufuata maadili kwa sababu utambulisho wowote wa taifa unaendana na maadili ya nchi husika.
Sheikh huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema vijana wengi wa kitanzania wametumbukia katika maadili ambayo hayaendani na jamii husika na kushindwa kufuata maagizo ya mwenyezi mungu hali ambayo inahatarisha ukuaji wa uchumi wa taifa ambao unategemea zaidi vijana.