Kaimu Kamanda mkoa wa Tanga mrakibu mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mayala Towo
Akizungumza katika eneo la tukio Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mayala Towo amesema shehena hiyo ilikuwa pia na mafuta ya kupikia kutoka ubeligiji, Sukari kutoka India na vipuri kutoka nchi tofauti za Ulaya.
Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) tawi la Tanga Bwana Samir Buelgaaba amekiri kuwa hali ya ukwepaji wa kodi katika bandari bubu ya Kigombe ni ya kutisha kwa sababu sehemu kubwa ya bidhaa zinazouzwa katika maduka mbalimbali katika baadhi ya maduka yaliyopo katika jiji la Tanga, Muheza na Mkinga zinatoka nje ambazo inadaiwa kuwa zimeingizwa nchini kinyume cha sheria.
Kufuatia hatua hiyo kaimu meneja wa forodha mkoa wa Tanga Bwana Jumbe Magoti amesema wazingatie sheria zilizowekwa katika zoezi la tozo za faini kisha watataifisha vyombo vilivyotumika katika usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka kisiwani Zanzibar kuingizwa bara bila kulipiwa ushuru.