Tuesday , 29th Sep , 2015

Wizara ya elimu nchini Tanzania imezindua utoaji wa elimu kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo inatarajiwa kuanza kutumika kwa wanafunzi wa shule za msingi kuanzia darasa la kwanza mpaka la tatu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sifuni Mchome na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shule,Marystella Wassena.

Akizungumza jijini Dar es salaam katibu mkuu wizara ya elimu nchini Tanzania Prof. Sifuni Mchome amesema kutokana na TEHAMA kutumika katika nyanja mbalimbali na kuwa wizara imeamua kuanzia kuitumia katika ngazi ya nchini ya elimu ili kutoa fursa za kusoma na ubora wa elimu.

Kwa upande wake afisa mradi wa mpango wa kukuza kusoma na kuandika Bi. Agripina Habichi amesema mradi huo utaweza kufika hadi maeneo ya vijijini ambapo hakuna umeme kwakuwa baadhi ya vifaa vitakavyotumika vitakuwa vinatumia mionzi ya jua katika kujiendesha.

Bi. Habichi amesema kufanikiwa kwa mpango huo kutasaidia katika kuharakisha, kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma za elimu kwa wanafunzi katika ufundishaji.