Friday , 13th Jun , 2014

Bajeti Kuu ya serikali ya Tanzania ya Sh. Tr.

Waziri wa fedha na uchumi wa Tanzania Bi. Saada Mkuya Salum.

Bajeti Kuu ya serikali ya Tanzania ya Sh. Tr. 19.87, imewasilishwa jana Bungeni na waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, huku ikiwabana wananchi katika bidhaa za huduma za starehe, na kipaumbele kikubwa kikiwa Elimu ikiwa na tril 3.5.

Aidha katika Bajeti hiyo, badala ya serikali kupata fedha kutoza kodi bidhaa za muhimu kwa wananchi kama mafuta, safari hii wananchi hawajaguswa katika huduma na bidhaa muhimu kwao, na badala yake fedha nyingi zinatarajiwa kukusanywa baada ya kufuta misamaha ya kodi.

…...........................
Kwingineko Afrika mashariki nchini Kenya na Uganda bajeti za mwaka wa fedha 2014/2015 ziliwasilishwa bungeni, Uganda ikiwasilishwa na Waziri Maria Kiwanuka mabapo sekta ya Ujenzi na Usafiri ilionekana kuchukua sehemu kubwa ya bajeti hiyo ya Tril. 14 ya nchini Uganda.

Nchini Kenya Bajeti hiyo ilisomwa na Waziri mwenye dhamana Henry Rotich, kubwa likiwa ni kuanzishwa kwa manunuzi ya Umma kwa njia ya mtandao ili kudhibiti ufujaji wa fedha katika michakato ya manunuzi na kuhakikisha fedha inakuwa na thamani zaidi nchini Kenya.