Tuesday , 24th May , 2016

Serikali imesema kuwa imetenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kuwapatia vijana mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha kujiajiri na kuajiriwa katika sehemu mbalimbali ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini.

Waziri nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama.

Akitolea ufafanuzi juu ya utatuzi wa tatizo hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu Mhe.Jenista Mhagama, amesema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha kupata ajira kwenye viwanda vilivyopo na vinavyotarajiwa kujengwa nchini.

Mhe. Jenista amesema kuwa serikali inatambua tatizo la ajira linaliowakabili vijana nchini hivyo serikali imeamua kutenga bajeti maalumu kupitia wizara hiyo ili kutatua changamoto hiyo ambayo inawakabili vijana wengi nchini kutokana kukosa ujuzi wa kujiajiri au kuajiriwa.

Awali akijibu swali hilo la serikali imejipangaje kuwapatia mafunzo vijana ili kuweza kupata ajira au kujiairi wao wenyewe, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa Shirika la Viwanda vidogo linajukumu la kusimamia wajasiriamali wadogo kujikwamua kiuchumi.