Wednesday , 13th Jan , 2016

Naibu waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi mhe. William Ole Nasha, amemuagiza msajili wa vyama vya ushirika nchini kuunda tume itakayotoa majibu juu ya mgogoro unaoendelea ndani ya chama cha msingi cha wakulima wa tumbaku cha Mpanda mkoani Katavi.

Naibu waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi mhe. William Ole Nasha

Kabla ya kutoa agizo hilo Naibu waziri huyo alimtaka afisa ushirika wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Bw. Laxford Mbunda, atoe maelezo kuhusu deni la zaidi ya shilingi milioni 200 linalokikabili chama hicho cha msingi cha wakulima wa tumbaku cha Mpanda kati

Baada ya kusikiliza maelezo ya Mwenyekiti Naibu waziri Ole Nasha akatoa agizo hilo kwa msimamizi mkuu wa vyama vya ushirika nchini, huku akiwataka wanachama wawe watulivu kwa lengo la kukinusuru chama hicho muhimu kwa shughuli zao za kilimo.