Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mh Nape Nnauye
Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mh Nape Nnauye amesema hatua hiyo inakuja baada ya kuwataka wamiliki wa magazeti 570 mwaka 2013 kuanza kuchapisha magazeti hayo vinginevyo yatafutiwa usajili baada ya miaka mitatu.
Mhe. Nnauye ameongeza kuwa nchini kuna magazeti 881 yaliyosajiliwa huku mengi yao yakiwa hayachapishwi licha ya kusajiliwa hivyo serikali imeanza kuchukua hatua na wanatarajiwa kuanza kuangazia vyombo vingine.






