Friday , 26th Sep , 2014

Serikali ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu Kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari Saed Kubenea kutaka tafsiri ya baadhi ya vifungu vya sheria ya mabadiliko ya katiba kuhusu Mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba kuiboresha rasimu.

Jaji mkuu wa Tanzania, Frederick Werema asikisitiza jambo bungeni.

Akizungumza leo Bungeni Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredrik Werema amesema kuwa ni kweli kulikua na matatizo ya kilugha katika vifungu ambavyo viliombewa tafsiri lakini mahakama imekubali kuwa Bunge hilo lina mamlaka ya kuboresha na kuibadili rasimu hiyo lakini kwa mipaka maalumu.

Jaji Werema amesema Mahakama haina mamlaka ya kuamua kiwango ambacho bunge maalumu la katiba linaweza kuboresha rasimu ya katiba kwa kuwa jambo hilo ni jambo la kisiasa zaidi kuliko sheria.

Awali Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la katiba Mh. Samweli Sitta akimkaribisha Jaji mkuu kwa ajili ya kufafanua hukumu hiyo alisema kuwa vyombo vingi vya habari vimeshindwa kuifafanua hukumu hiyo na kuupotosha wananchi juu ya hukumu hiyo.