
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati akisoma muelekeo wa hali ya uchumi kwa mwaka fedha uliopita 2017/2018 na mpango wa taifa kwa mwaka wa fedha 2018/2019, ambapo amesema jitihada za kupunguza umasikini nchini zimepiga hatua kutoka asilimia 24.6 hadi kufikia asilimia 16 mwaka 2016 na bado serikali inaendelea na mpango wa kupunguza.
"Katika mpango wa taifa wa mwaka uliopita umeonyesha mafanikio ya kimaendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo kiwango cha upatikanaji wa umeme, maji na huduma zingine za kijamii zimeongezeka huku miradi mingine ya maendeleo ikiendelea kutekelezwa", amesema Dkt. Mpango.
Katika hatua nyingine, Dk. Mpango amesema ili kufanikisha mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019, serikali imeelekeza nguvu katika miradi minne mikubwa ikiwemo, kuendeleza mradi wa makaa ya mawe (Kiwira), kiwanda cha kufua chuma (Mchuchuma), Shamba la Miwa, eneo la wazi la uwekezaji la Kurasini pamoja na kuunganisha uchumi na maendeleo ya wananchi