Tuesday , 9th Feb , 2016

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini uliofanyika , jijini Dar es Salaam.

Mhe. Majaliwa amesema maeneo yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka na yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na usafirishaji.

Amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi inamilikiwa na Watanzania wenyewe.

Katika Mkutano huo Waziri Mkuu pia alizindua Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.