Thursday , 30th Apr , 2015

Serikali imesema itaelekeza nguvu zake katika hifadhi za wanyama ya Ruaha na Rungwe ili kudhibiti suala la ujangili.

Waziri wa maliasili na Utalia Lazaro Nyarandu akiwa katika kikao na Viongozi wa Mkoa wa Iringa wa kwanza kushoto ni Waziri wa Ardhi Nymba na maendeleo ya Makazi mh Wiliam Lukuvi.

Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu amesema kuwa ili kufanikisha suala hilo atahakikisha kuwa vitendea kazi na rasirimali watu vinapatikana.

Waziri ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa iringa pamoja na viongozi wa msitu wa mbomipa katika ukumbi wa siasa ni kilimo.

Naye waziri wa aridhi nyumba na makazi William Lukuvi amemuomba waziri wa maliasili na utalii kulifanyia kazi ombi la watumishi wa hifadhi waliomo ndani ya hifadhi kwenda kuishi nje ya hifadhi.

Akijibu ombi hilo waziri wa maliasili amesema kuwa tayari serikali inafanyia mkakati wa kuwajengea nyumba nje ya hifadhi.

Hata hivyo waziri amefanya ziara katika msitu wa mbomipa uliopo katika manispaa ya Iringa na ameidhinisha kutumika kwa msitu huo kama hifadhi.