Wednesday , 8th Jun , 2016

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo inawasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017, ambayo inatarajiwa kuwa ni zaidi ya shilingi trilioni 29.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,

Bajeti hiyo itawasilishwa leo mjini Dodoma, na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, huku kati ya vipaumbele vinavyotajwa kuwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa Maendeleo ya taifa wa mwaka 2016/2017 wa miaka mitano.

Aidha vipaumbe vingine ni pamoja na ukusanyaji wa mapato pamoja na uimarishaji wa viwanda ambavyo vitasaidia kukuza uchumi wa nchini na kuifikisha kati nchi zitakazokuwa na uchumi wa kati.

Bajeti hiyo pia inaweka mkazi zaidi katika ukamilishaji wa miradi inayoendelea kutekelezwa miradi mipya, ulipaji wa madeni yaliyohakikiwa pamoja na utekekelezaji wa maeneo yote ya vipaumbele yaliyoainishwa katika mpango wa maendeleo wa mwaka wa fedha 2016/2017.

Bajeti hiyo itawasilishwa majira ya Alasiri, muda ambao pia nchi nyingine za afrika Mashariki zitawasilishwa utaratibu ambao nchi hizo za Jumuiya ya Afrika Mashariki umejiwekea kuwasilisha bajeti zao kwa pamoja.