Friday , 17th Jun , 2016

Waziri wa afya, jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu imeahidi kuendelea na ujenzi wa jengo la X Rays katika hospitali ya rufaa ya Mbeya ambalo lilianza ujenzi wake Novemba 9 2012.

Hayo yamesemwa Bungeni na Waziri wa Afya kufuatilia swali la Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aliyetaka kujua ni lini serikali itakamilisha ujenzi wa jengo hilo ili kuondoa adha kwa wagonjwa.

Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema kwamba jengo hilo limetengewa bilioni 5 ambapo 3 zitamlipa mkandarasi na 2 zitatumika kuanza kununua vifaa tiba vya hospitali hiyo.

Aidha Waziri amebeinisha kuwa zimetengwa bilioni 9 kwa ajili ya kusaidia vifaa tiba katika baadhi ya hospitali za rufaa nchini ili kuziwezesha kuweza kutibu wagonjwa wanaohitaji huduma katika maeneo yao.