Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Akiongea bungeni leo Dodoma katika kipindi cha Maswali na majibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, amesema serikali imeshapata pesa ya kununulia vifaa hivyo kwa ajili ya hospitali hizo.
Mhe. Mwalimu amesema kuwa suala hilo limechelewa katika utekelezaji wake kutokana na kutokua na pesa na rais tayari ameshatoa pesa kutoka katika fedha zilizokuwa zitumike kwa ajili ya semina elekezi ya mawaziri ili kununulia vifaa tiba hivyo.
Mhe Ummy Mwalimu ameongeza kuwa tatizo hilo la kusambaza vifaa tiba wataweza kulitekeleza kabla ya Mwaka wa fedha ujao ili kuwaondolewa wananchi mzigo mkubwa wa vipimo kutokana na serikali kukosa vifaa tiba hivyo.
Waziri Ummy Mwalimu alitoa ufafanuzi wa jambo hilo baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Kemilembe Julius alietaka kujua ni lini serikali itafunga vifaa tiba hivyo katika hospitali ya rufaa ya Sekou toure iliyopo jijini Mwanza.