Friday , 26th Jun , 2015

SERIKALI inakusudia kufanya upya sensa ya tembo, kati ya Agosti na Septemba mwaka huu, katika ikolojia ya Ruaha-Rungwa ili kupata idadi kamili ya wanyama hao ambao wanatishia kupotea kutokana na ujangili.

Mizoga ya Tembo 13 waliouawa na kung'olewa meno na majangili katika pori la Akiba la Piti kata ya Ngwara wilayani Chunya mkoani Mbeya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Adelhem Meru , alipokuwa akizungumza leo jijini Arusha, katika kongamano la utalii Afrika.

Kongamano hilo limeandaliwa na vijana wa kitanzania, kwa lengo la kukutanisha wadau wa utalii ili kulinda rasilimali kwenye hifadhi za taifa barani Afrika.

Amesema kuna umuhimu wa kufanya sense upya, kutokana na sense iliofanyika mwaka 2013 ilipata tembo 20,000, lakini mwaka 2014 idadi ya tembo ilipungua na kufika tembo 8,000, hivyo tembo 12,000 hawajulikani walipo.

Dk Adelhem amesema ujangili ni tishio katika sekta ya utalii, kwani wanyama wakiisha kuna hatari kusababisha ukosefu wa ajira, ambao hadi sasa watu 700,000 wameajiriwa na idadi hiyo inaongezeka.

Amesema nchi nyingi za Afrika mapato yake ynategeema sekta za utalii, hivyo bila kuilinda kwa kupambana na ujangili w auharibifu mazingira, vyanzo vya maji na ujangili ni hatari kwa uchumi wa nchi hizo.

Akitoa mfano amesema Tanzania peke yake inaingiza zaidi ya shilingi bilioni 2.06 katika mapato yake ya kigeni.

Aidha alisema katika kupambana na ujangili Tanzania kupitia marafiki zake, wamenunua ndege na vifaa vya kupambana na ujangili ili kuwalinda wanyama hao.

Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa,(TANAPA) Allan Kijazi, alisema wao katika kupambana na ujangili na kuhakikisha shirika hilo linakuwa endelevu, kila mwaka wanatenga bajeti ya shilingi bilioni 70 ambayo inatumika kwenye doria, ununuzi wa vifaa na ukarabati miundo mbinu.