Katibu Mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
Akizungumza Jijini Dar es salaam jana Katibu Mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema kampuni hiyo ndiyo iliyotumika kama wakala wa ununuzi wa dhamana wa serikali zenye thamaniya trilioni 1.2 katika serikali ya awamu ya nne.
Balozi Sefue amesema kuwa serikali inawachunguza wamiliki wa kampuni hiyo akiwemo Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzani TRA, Harry Kitilya, pamoja na Marehemu Fraten Mboya na Gasper Njuu.
Aidha Katibu Mkuu huyo amesema Tanzania ilikopa fedha hizo kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya kawaida kutoka Bank Standard kupitia benki ya Stanbic na ada yake ilikuwa ni asilimia 1.4 lakini iliongezwa asilimia 1 zaidi fedha ambazo hazikuwemo kwenye makubaliano.
Balozi Sefue amesema kuwa akaunti ya kampuni ya EGMA inayodaiwa kumilikiwa na Kitilya na wenzake iliyopo benki ya Stanbic Tanzania ilingiziwa dola za kimarekani milioni 6 na zote zilitolewa mara moja.
Aidha ameongeza kuwa Rais Magufuli ameagiza kwamba fedha hizo zitakapopatikana kama atakuwa hajateua baraza la mawaziri makatibu wakuu watakaa kupanga matumizi yake.