
Akizungumza katika kikao cha bunge la bajeti Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya amesema kwa kuanzia serikali itatoa kiasi cha shilingi bilioni 57 kwa ajili ya kulipa madeni yanayodaiwa na kufuatiwa na ongezeko la bilioni 200.
Hata hivyo Mhe. Mkuya amesema kwa sasa wameanza kufanya utaratibu wa kuchuja wafanyakazi na kuwahamisha katika maeneo mbalimbali ili kuiongeza ufanisi haswa katika ukusanya wa kodi na kuwa wameandaa mkakati wa kusaidia kuinua thamani ya shilingi dhidi ya dola.
Akizungumzia kuhusiana na suala la kushuka thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola Mkuya amesema wameandaa semina elekezi ambayo itawakutanisha wabunge na wadau mbalimbali wa biashara ili kuweza kuweka mikakati ya kuiinua shilingi ya Tanzania ikiwemo kupunguza matumizi ya dola katika bidhaa za ndani.
Kwa upande wa benk kuu wamefanikiwa kuingiza dola katika mzunguko wa fedha na kuwa wamebaini kuwepo na mchezo mchafu kwa benki za biashara nchini wa kuzinunua dola na kuzipandisha ili waweze kupata faida katika ubadilishaji wa fedha za kigeni.