Thursday , 13th Aug , 2015

Naibu waziri wa Nishati na madini , Mh. Charles Kitwanga ametembelea eneo la mradi la mto mkuju litakalochimbwa madini ya urani katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma na kuwaahidi wananchi ifikapo april mwaka 2016 mradi utaanza kuzalisha.

Naibu waziri wa Nishati na madini anae shughulikia Madini, Mh. Charles Kitwanga

Waziri Charles Kitwanga ametembelea eneo hili la mradi wa uchimbaji wa madini ya urani katika wilaya ya namtumbo mkoani Ruvuma, pamoja na kuwatoa hofu wananchi kwamba hakuna madini ya urani yanayochimbwa na kuondolewa kinyemela lakini pia anasema wizara ya nishati na madini ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha makubaliano ya kuanza rasmi uzalishaji ifikapo april 2016.

Utafiti wa madini ya urani katika eneo la mto mkuju lenye ukubwa wa kilomita za mraba 20,000 ndani ya hifadhi ya Selou ambao unasimamiwa na kampuni ya mantra tanzania, tangu mwaka 2007 tayari umeshafanya uwekezaji wa dola za marekani milioni 200 huku matarajio ikiwa ni kufikia uwekezaji wa bilioni moja ambapo pia mapambano dhidi ya ujangili wa wanyama-pori waliopo kwenye hifadhi ukiwekewa mkazo mkubwa .

Pamoja na waziri Kitwanga kutembelea eneo la mradi wa urani mto Mmkuju, pia amekagua baadhi miradi inayofadhiliwa na Mantra Tanzania kwa wakazi wa namtumbo ikiwemo maabara na maktaba ya kisasa kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari selou iliyopo kijiji cha likuyusekamaganga.