Monday , 6th Jul , 2015

Serikali imeombwa kusimamia sera na sheria za kuwawezesha wananchi nchini Tanzania ili nchi ifikie uchumi wa kati ikiwa ni pamoja na wawekezaji wazawa kupewa kipaumbele kuliko wageni.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini TPSF Dkt. Reginald Mengi wakibadilishana Mawazo.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi nchini TPSF, Dk. Reginald Mengi katika mkutano wa wafanyabiashara uliokua una lengo la kujadili changamoto zinazowakabili.

Dkt. Mengi amewataka wananchi kuuona umasikini kama sehemu ya changamoto na kuwa na imani ya kuushinda huku akiwataka wafanyabiashara kushikamana ili kupiga hatua ya kujiletea maendeleo.

Kwa upande ake mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania JWT, Johnson Minja ameomba mradi wa soko la kurasini utumiwe na wafanyabiashara wazawa ili kuiletea nchi maendeleo.