Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi nchini Anjelina Mabula amesema serikali inaandaa mswada wa sheria wakusimamia sekta ya uendelezaji milki ardhi nchini.
Waziri Mabula ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam alipokutana na wadau na wafanyabiashara wa uendelezaji milki nchini ambao walikutana kwa lengo lakujadili mambo mbalimbali yanayokwamisha uwekezaji katika ardhi nchini.
Amesema mamlaka hiyo itahusika na kusajili miradi ya ujenzi na mauzo ya majengo,na kusimamia mahusiano baina ya wapangaji na wenye nyumba sambamba na mikataba ya upangaji.
Kwa upande wao wataalamu,watumiaji na wamiliki wa ardhi nchini wamesema kwa mwaka zinahitajika nyumba laki mbili hali ambayo kwa sasa kama taifa bado hatujafikia hayo malengo.

