Wednesday , 3rd Aug , 2016

Waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo amesema serikali imetenga Dola Milioni 3 zaKimarekani kwa ajili ya lukuzu ya awamu ya tatu kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini na pesa hizo zinaanza kupelekwa Mpanda mkoani Katavi.

Waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo amesema serikali imetenga Dola Milioni 3 za Kimarekani kwa ajili ya ruzuku ya awamu ya tatu kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini na pesa hizo zinaanza kupelekwa Mpanda mkoani Katavi.

Prof.Muhongo ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam kwenye kikao kilichowakutanisha maafisa madini na wachimbaji wadogo wa madini ya Jas na makaa ya mawe lengo likiwa ni kutafuta suluhisho la matatizo yao ambayo yanapelekea kuzalishwa kwa madini hayo chini ya kiwango.

Prof.Muhongo amesema pesa hizo nikwa ajili ya wachimbaji wadogo wanaotambuliwa na serikali na kukemea maafisa wa serikali ambao wamekua wakidhulumu pesa za walengwa kwa kuweka majina ya ndugu zao ili waibe pesa hizo kinyume cha sheria.

Prof.Muhongo amesema katika kuhakikisha serikali inawasaidia wachimbaji wadogo wanazalisha kwa tija wameanza kutoa elimu kwa wachimbaji hao ili waweze kuchimba kwa tija na kwa faida kubwa ili pato la taifa liongezeke.

Amesema wameanza kuwafundisha wataalamu wa makaa ya mawe nchini ili wakajifunze namna ya kuzakisha kitaalamu siku za baadae ili yaje kutumika katika kuzalisha umeme na kuyatumia viwandani kutengeneza vitu mbalimbali.