Rais Magufuli
Tukio hilo limetokea leo wakati Rais Magufuli akiwa kwenye ziara mkoani Njombe alieleza kuwa, "huwezi ukawa RPC na bado watoto wa wenzako wanapotea umekaa tu ofisini na nyota zako mbona mtoto wako hawajapotea?. Kuanzia sasa hivi OCD wa hapa sio OCD tena, najua upo hapa unanilinda".
Akikazia kuhusu msimamo wake kwenye mauaji ya Njombe Rais Magufuli alimuonya Mkuu wa Mkoa na Wilaya huku akitaka wajitathmini
"Na hili suala la watoto kuuawa likijitokeza tena ujue kuwa mtaondoka wote kuanzia RC, ma DC, wenyeviti mpaka Mwenyekiti wa CCM Mkoa, wananchi wa Njombe acheni imani potofu za kishirikina".
"Njombe mmelitia doa taifa, kwa hili naomba tufanye toba watanzania wote nikiwemo na mimi ninayeongoza watanzania wanaoua wenzao", ameongeza
Baada ya toba
Muda mfupi baada ya kumalizika kwa toba, Rais Magufuli amesema. "nimeamua kumsamehe OCD haya rudi kazini. Yuko wapi?".





