Sunday , 31st Mar , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemteua Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayoishughulikia Sera, Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Nduguru.

Rais Magufuli

Awali nafasi aliyoteuliwa Bw. Nduguru ilikuwa wazi.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kwamba Nduguru alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Kufuatia Uteuzi  huo Rais Magufuli amemteua Bw. Msafiri Lameck Mbibo kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Mbibo alikuwa Meneja wa TRA mkoani Kilimanjaro.

Hata hivyo imeeelezwa kwamba, uteuzi wa viongozi hao unaanza mara moja leo Tarehe 31, Machi 2019