Tuesday , 3rd Feb , 2015

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck ambaye anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja kisiwani Zanzibar siku ya Jumatano anakuwa Rais wa kwanza kuwasili Zanzibar kwa kutumia usafiri wa baharini na kutotumia usafiri wa magari wakati wa mapokezi.

Maandalizi yakiendelea bandarini

Rais wa  Ujerumani  Joachim Gauck ambaye anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja kisiwani Zanzibar siku ya Jumatano anakuwa Rais wa kwanza kuwasili Zanzibar kwa kutumia usafiri wa baharini na kutotumia usafiri wa magari wakati wa mapokezi.

Kwa mujibu wa taarifa ya ikulu iliyotolewa mjini Zanzibar  na kusambazwa kwa vyombo vya habari kupitia mkuu wa mkoa  wa Mjini  Magahribi  Abdullah Mwinyi amesema kiongozi huyo atapokolewa bandarini Zanzibar na mwenyeji wake Dkt Ali Mohmaed Shein na kupigiwa mizinga 21 kwa heshima yake  na badaye kuanza msafara wake kwa miguu huku akisalimia wananchi kuelekea hoteli ya Serena iliyoko umbali wa kilomita moja..

Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema akiwepo hapa Zanzibar atapata fursa ya kuonana na viongozi wa dini  na kufanya nao mazungumzo huku mke wake Bi Daniela Schadt akifungua shule ya maandalizi  ya Herrn hunter Academy iliopo Mwera  wilaya ya Magharibi.

Ujio wa kiongozi huyo kwa kutumia usafiri wa boti umesababisha  barabara  itakayotumika kuanza kukarabatiwa na usafi na ulinzi kuimarishwa bandarini huku utaratibi  wa kuingia na kutoka bandarini ukiwa sio wa kawaida ..