Thursday , 5th Feb , 2015

Rais  wa  Ujerumani  Joachim  Gauck leo amehitimisha ziara yake nchini Tanzania kwa kutembelea makao makuu ya mahakama ya Afrika Mashariki inayoshughulikia haki za binadamu na Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck na Rais wa Mahakama ya Afrika Jaji mstaafu Agustino Ramadhani

Katika ziara hiyo Rais Gauck amezishauri  nchi  za  jumuiya  ya afrika  mashariki   kuendelea  kuimarisha  ushirikiano  miongoni  mwao    ikiwa  ni pamoja  na  kukabiliana   na  changamoto   zilizopo   bila  kukata tamaa  na  pia   kuimarisha   misingi  ya  haki   za  binadamu.

Wakizungumza    baada  ya  kumaliza  mazungumzo  ya  faragha  na Rais huyo,  Rais  wa  mahakama  ya  Afrika jaji  mstaafu   Agusitino  Ramadhani    na  katibu  mkuu   wa  jumuiya  ya  Afrika  Mashariki   dr. Richard  Sezibera  pamoja  na  kuishukuru  Ujerumani  kwa  misaada,   wamesema  ziara   hiyo  imefungua  ukurasa  mpya  wa  ushirikiano    na  imeongeza  chachu ya  maendeleo.

Kwa  upande  wao  Naibu  Katibu  mkuu  wa EAC  anayeshughulikia   miundombinu  bi  Jeska  Erio  , spika wa  bunge  hilo  Daniel  Kidega, na  waziri  wa  Afrika  Mashariki  wa  Tanzania Dkt Harison Mwakyembe  wamesema  kuwa Ujerumani  ni  miongoni  mwa  nchi  chache  duniani  zinazoonesha  kwa  vitendo  nia ya  kuzisaidia  nchi  maskini   zikiwemo   za  Afrika  Mashariki  na  itakazoendelea  kukumbwa   na   wananchi  wote  wa  nchi  wanachama.

Kiongozi  huyo   amemaliza  ziara yake  nchini  kwa  kutembelea  hifadhi ya taifa  ya serengeti    hatua  ambayo  pia  inatarajiwa  kusaidia  kuhamasisha  na  kuvutia  watalii  kutoka  ujerumani