Tuesday , 29th Nov , 2016

Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye amesema kwamba amelitaka bunge la nchi hiyo kumsaidia njia sahihi ya kujiuzulu.

Park Geun-hye

Amesema ameliachia bunge la nchi hiyo kuhusu hatima yake ikiwa ni pamoja na kukatisha muhula wa utawala wake na kuainisha kwamba hataki kuacha ombwe la mamlaka.

Rais  Park anakabiliwa na shinikizo la kumtaka ajiuzuru huku uchunguzi ukiendelea kubaini endapo alimruhusu rafiki yake wa zamani kuwa na ushawishi kisiasa kwa manufaa yake.

Bunge la nchi hiyo linakutana Ijumaa wiki hii kujadili ikiwa Rais huyo atakabiliwa na kupigiwa kura ya kuondolewa madarakani.

Baadhi ya wabunge kutoka chama tawala wanataka Rais huyo ajiuzulu kwa heshima huku upinzania ukidai kuwa Rais huyo anajaribu kukwepa  kuondolewa madarakani.