Sunday , 27th Jan , 2019

Kesho Jumatatu Wakuu wa Mikoa wote nchini wametakiwa kufika kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, kwa ajili ya kutoa taarifa ya ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo baada ya kukabidhiwa Desemba 10 mwaka uliopita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Wito huo umetangazwa Jijini Dodoma na Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ambapo amesema Wakuu wa Mikoa wote wametakiwa kuwa jijini Dar es Salaam kesho kujieleza kwa Rais John Magufuli kuhusu vitambulisho walivyopewa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo.

Waziri Jaffo amesema, “tumewaandikia barua wakuu wa mikoa watoe maelezo juu ya ugawaji vitambulisho, namna lilivyofanyika. Lakini majibu watawasilisha wenyewe mbele ya Rais.”

Katika suala la vitambulisho kuna mikoa bado imegawa kwa asilimia mbili na nne wakati wengine wameshafika zaidi ya asilimia 94. Lazima tukazungumze na kujua changamoto ni nini na tunatokaje,” amesema Jafo.