Saturday , 10th Sep , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Eliya Ntandu na wakurugenzi wa Halmashauri 13 nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli

Akitangaza majina hayo Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema nafasi ya katibu wa mkoa wa Songwe ilikuwa wazi hivyo nafasi hiyo imejazwa leo.

Wakati huo huo Rais Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa Halmashauri 11 pamoja na Mkurugenzi wa Mji mmoja na Manispaa mmoja ili kujaza nafasi zilizokuwa zimeachwa wazi.

Walioteuliwa ni kama ifuatavyo

1. Godwin Emanuel Kunambi Manispaa ya Dodoma

2. Elias R. Ntirihungwa Mji wa Tarime

3. Mwantum Dau Halmashauri ya Bukoba

4. Frank Bahati Halmashauri ya Ukerewe

5. Hadson Stanley Kamoga Halmashauri ya Mbulu

6. Mwaila Sith Pangani Halmashauri ya Nsimbo

7. Godfrey Sanga Halmashauri ya Mkalama

8. Yusuph Daud Semuguruka Halmashauri ya Ulanga

9. Bakari Kasinyo Mohamed Halmashauri ya Nachingwea

10. Juma Ally Mnwele Halmashauri ya Kibondo

11. Butamo Nuru Nalahwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

12. Waziri Mourice Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

13. Fatuma Omary Latu Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo