Saturday , 26th Apr , 2014

Tanzania leo inasherehekea miaka 50 ya Muungano wa kihistoria wa Tanganyika na Zanzibar na sherehe za maadhimisho hayo zimefanyika uwanja wa taifa kwa gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama na kukaguliwa na amiri jeshi mkuu Rais Jakaya Kikwete.

Rais Kikwete wa Tanzania.

Akizungumza na wanainchi kupitia vijana katika Ukumbi wa PTA, jijini Dar es salaam jana, Rais Jakaya Kikwete alisema Muungano uko salama na kusisitiza hana shaka utaendelea kudumu na kwamba wale wachache wanaouchukia na wanaotaka uvunjike wana lao jambo.

Akizungumzia mchakato wa kuunda katiba mpya, Rais Kikwete alisema dhamira yake ilikuwa kutoa fursa kwa watanzania kujadili kwa kina na upana na kutambua yale ya msingi yanayohitaji kuingizwa katika Katiba ikiwa ni pamoja na kuondoa kero zilizobaki za Muungano.

Rais alisema waasisi walikuwa mstari wa mbele kutanguliza maslahi ya nchi mbele kwa manufaa ya wananchi wote hivyo muungano hauna budi kulindwa kwa nguvu zote.