Wednesday , 6th Jan , 2016

Wizara ya Mambo ya Ndani imetangaza kuanza kwa operation maalum ya kuwakamata na kuwarudisha makwao raia wote wa kigeni wanaoishi bila vibali nchini pamoja na kufanya kazi zinazoweza kufanywa na wananchi wazawa.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara katika idara ya a uhamiaji Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni lengo ni kuwabaini raia wa kigeni waliopo nchini kinyume cha sheria pamoja na kufanya kazi zinazoweza kufanywa na wazawa.

Akizungumzia hali ya wahamiaji katika jiji la Dar es salaam kamishina wa uhamiaji wa mkoa wa Dar es Salaam John Msumule amesema wanatarajia kukamata wageni 350 katika kampeni inayoanza leo huku wakiwa tayari wengine wamefikishwa mahakani na kurudishwa katika nchi zao.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri Masauni amesema serikali ipo mbioni kuanza mchakato wa kuanzisha mahakam ya kijeshi ili kuwashughulikia maofisa uhamiaji wanaobainika kujihusisha na rushwa na kuichafua idara hiyo .