Raia wa Afrika ya Kusini Guguleth Mathebula Zulu (38) aliyefika nchini kwa utalii a kupanda mlima kilimanjaro amefariki leo baaada ya kupatwa na tataizo la kushindwa kupumua kwenye mwinuko wa juu mlimani.
Shirika la hifadhi ya Taifa TANAPA kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za serikali zinaendelea na utaratibu wa kurejesha mwili wa marehemu nchini Afrika ya kusini kwaa ajili ya taratibu za maziko.
Zulu alifika nchini na kuanza kupanda mlima Kilimanjaro tarehe 14.07.2016 kwa ajili ya kuenzi jitihada za rais wa kwanza wa Africa ya Kusini Nelson Mandela za kusaidia familia masikini nchini Afrika ya Kusini, hususani kuwapatia mahitaji muhimu watoto wa kike ambao hawana uwezo wa kupata mahitaji muhimu.
Hii ni mara ya pili kwa watalii kutoka Afrika ya kusini kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuenzi juhudi za Mandela katika kusaidia jamii ya watoto wa kike kupitia kampeni maalumu ya kupanda mlima Kilimanjaro.







