Monday , 20th Jun , 2016

Magavana kutoka nchi zilizopo katika taasisi ya usimamizi wa fedha na uchumi kusini na mashariki mwa Africa (MEFMI ) wamepongeza hatua ya Shirika la Fedha Duniani IMF kuingiza pesa ya China Yuan kwenye orodha ya pesa duniani.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo gavana wa benki ya kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu amesema Yuan kuruhusiwa na IMF itaongeza akiba ya nchi katika fedha za kigeni ikizingatiwa kuwa asilimia 5 ya pesa hiyo ni ya china.

Prof. Ndulu amesema kwa sasa wafanyabiashara wa Tanzania na China na shughuli za kibiashara na uwekezaji hawatalazimika tena kutumia dola ya kimarekani kutokana na Yuan kupanda thamani

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MEFMI Caleb Fundamba amewataka magavana waliohudhuria mkutano huo kuhakikisha kuwa wanapambana na rushwa ili miradi ya kimaendeleo iweze kufanikiwa nakuifanikisha afrika kuachana na kuomba misaada.

Fundamba amesema, Africa ina utajiri wa raslimali ndio sababu nchi za nje huja barani humu kuwekeza lakini bila viongozi wa Africa kupambana na rushwa hata pesa za misaada ya kuendesha miradi itatumika ovyo hali ambayo itaifanya afrika kuzidi kuwa ombaomba.